Original Language
Swahili
ISBN (PDF)
978-92-9268-396-2
Number of Pages
100
Reference Number
PUB2022/083/L
Date of upload

05 Sep 2022

World Migration Report 2022: Chapter 3 (Swahili)

Ripoti Hii Ya Uhamiaji Duniani Ya 2022: Uhamiaji na wahamiaji: Sifa na maendeleo ya kikanda
Also available in:

Sura ya 3 inatoa majadiliano ya sifa muhimu za kikanda za, na maendeleo katika, uhamiaji. Mjadala huo unazingatia kanda sita za ulimwengu, yaani Afrika, Asia, Ulaya, Amerika ya Kusini na Karibiani, Amerika ya Kaskazini na Oceania.  Kwa kila moja ya kanda hizi, uchambuzi unahusisha: 

  1. Maelezo ya kijumla na majadiliano mafupi ya takwimu muhimu za uhamiaji wa watu ulimwenguni pamoja na data ya usafiri wakati wa UVIKO-19, iliyogawanywa katika kiwango cha kikanda; na
  2. Maelezo mafupi na dhahiri ya "sifa na maendeleo muhimu" kuhusu uhamiaji katika ukanda huo, yakizingatia data, habari na uchambuzi anuwai, pamoja na yale yanayotoka kwa mashirika ya kimataifa, watafiti na wachambuzi.

Kwa ujumla, sura hii inazungumzia tofauti muhimu katika kanda na kanda ndogo mbalimbali, pamoja na uchangamano unaoongezeka katika mienendo ya uhamiaji ulimwenguni. Tofauti na uchangamano huu unasisitiza mfanano na tofauti za msingi katika mienendo ya uhamiaji ya muda mrefu, zikimulika nafasi na changamoto muhimu na changamoto katika utungaji wa sera za kimataifa na kiulimwengu.