alt
Original Language
Swahili
Number of Pages
20
Reference Number
PUB2020/102/L
Date of upload

06 Jan 2021

World Migration Report 2020 (Swahili): Chapter 1

Muhtasari wa ripoti: Kutoa taswira ya uhamiaji na mwendo katika nyakati zenye mashaka mengi
Also available in:

Uhamiaji wa kimataifa ni tukio changamano linalohusisha vipengele vingi vya kiuchumi, kijamii na kiusalama ulimwenguni kote. Katika sura hii ya muhtasari wa chapisho kuu la IOM, Ripoti ya Uhamiaji Duniani 2020, wasomaji wataweza kupata ufahamu kuhusu mienendo muhimu, data na habari kwa ufupi. Zaidi ya kuwa muhtasari mkuu wa ripoti hii, sura hii ya maelezo ya kijumla inaunganisha "taswira pana" ya kimkakati kuhusu mienendo ya uhamiaji na ufurushwaji na mageuzi mapana duniani yanayotokea kote ulimwenguni, hasa yanavyohusiana na utoaji habari (za kupotosha), mabadiliko ya kisiasa na teknolojia. 

Ripoti ya Uhamiaji Duniani 2020 inajaribu kutumia kusanyiko la data, utafiti na uchambuzi wa uhamiaji uliopo ili kusaidia kujenga msingi wa ushahidi juu ya maswala muhimu zaidi na ya dharura ya uhamiaji ulimwenguni wakati wa sasa. Kutokana na asili yake, mienendo changamano ya uhamiaji ulimwenguni haiwezi kupimwa, kueleweka na kudhibitiwa kikamilifu. Hata hivyo, kama ripoti hii inavyoonyesha, tunalo kusanyiko la data na habari zinazoendelea kukua na kuwa nzuri zaidi ambazo zinaweza kutusaidia "kuelewa vizuri" sifa za msingi za uhamiaji katika nyakati zenye mashaka zaidi. Ili kupata habari kuhusu mienendo na masuala ya uhamiaji ulimwenguni, Ripoti ya Uhamiaji Duniani 2020 ni rejeleo la kuaminika kuliko mengine.

International migration is a complex phenomenon that touches on a multiplicity of economic, social and security aspects all around the world. In this overview chapter of IOM’s flagship publication, the World Migration Report 2020, readers will be able to access key trends, data and information at a glance. More than just an executive summary of the report, the overview chapter links the strategic “bigger picture” on migration and displacement dynamics to broader global transformations occurring around the world, especially as they related to (mis)information, political change and technology.

The World Migration Report 2020 seeks to use the body of available data, research and analysis on migration to help build the evidence base on some of the most important and pressing global migration issues of our time. By their very nature, the complex dynamics of global migration can never be fully measured, understood and regulated. However, as this report shows, we do have a continuously growing and improving body of data and information that can help us “make better sense” of the basic features of migration in increasingly uncertain times. For information on migration trends and issues globally, the World Migration Report 2020 is an authoritative reference like no other.