Original Language
Swahili
ISBN (PDF)
978-92-9268-385-6
Number of Pages
47
Reference Number
PUB2022/082/L
Date of upload

05 Aug 2022

World Migration Report 2022: Chapter 2 (Swahili)

Ripoti Hii Ya Uhamiaji Duniani Ya 2022: Uhamiaji na wahamiaji: Muhtasari wa hali duniani
Also available in:

Sura hii inatoa maelezo ya kijumla ya data na mienendo ya ulimwengu mzima ya wahamiaji wa kimataifa na uhamiaji wa kimataifa. Pia inatoa majadiliano kuhusu vikundi maalumu vya wahamiaji - yaani wafanyikazi wahamiaji, wakimbizi, waomba hifadhi na wakimbizi wa ndani – pamoja na athari za UVIKO-19 kwa uhamiaji na mienendo ya muda mrefu ya utumaji fedha wa kimataifa. Zaidi ya hayo, sura hii inaangazia ongezeko la data ya programu na data zingine za IOM, hasa juu ya wahamiaji waliopotea, usaidizi wa kurejea nyumbani kwa hiari na kujumuishwa tena katika jamii, utoaji wa makazi mapya, na ufuatiliaji wa waliofurushwa.

Makadirio ya sasa ni kwamba kuna wahamiaji milioni 281 wa kimataifa ulimwenguni (au 3.6% ya idadi ya watu duniani). Huku idadi kubwa ya watu ulimwenguni ikiendelea kuishi katika nchi ambayo walizaliwa, watu wengi zaidi wanahamia nchi zingine, hasa zile zilizo katika ukanda wao. Wengine wengi wanahamia nchi zenye mapato ya juu ambazo ziko mbali zaidi, hata hivyo, UVIKO-19 ilisababisha usumbufu mkubwa kwa wahamiaji na mifumo ya uhamiaji, hasa katika sekta inayotegemea mipangilio ya hali ya juu ya uhamaji.  Kazi ndiyo sababu kuu ya watu kuhama kimataifa, na wafanyikazi wahamiaji huchangia idadi kubwa ya wahamiaji wa kimataifa ulimwenguni, huku wengi wakiishi katika nchi zenye mapato ya juu. Ufurushwaji kote ulimwengu umefikia kiwango cha juu sana, huku idadi ya wakimbizi wa ndani ikiwa kama milioni 55 na idadi ya wakimbizi ikiwa zaidi ya milioni 26.

This chapter provides an overview of global data and trends on international migrants and international migration. It also provides a discussion of particular migrant groups – namely migrant workers, refugees, asylum seekers and IDPs – as well as of COVID-19 impacts on migration and long-term trends on international remittances. In addition, the chapter highlights the growing body of IOM programmatic and other data, particularly on missing migrants, assisted voluntary returns and reintegration, resettlement, and displacement-tracking.

Current estimates are that there are 281 million international migrants globally (or 3.6% of the world’s population). While the vast majority of people in the world continue to live in the country in which they were born, more people are migrating to other countries, especially those within their region. Many others are migrating to high-income countries that are further afield, however, COVID-19 caused significant disruptions to migrants and migration systems, especially in sector relying on high mobility arrangements.  Work is the major reason that people migrate internationally, and migrant workers constitute a large majority of the world’s international migrants, with most living in high-income countries. Global displacement is at a record high, with the number of internally displaced at around 55 million and the number of refugees at over 26 million.