alt
Original Language
Swahili
Number of Pages
98
Reference Number
PUB2020/104/L
Date of upload

06 Jan 2021

World Migration Report 2020 (Swahili): Chapter 3

Uhamiaji na wahamiaji: Sifa na maendeleo ya kikanda

Sura ya 3 inatoa majadiliano ya sifa muhimu za kikanda za, na maendeleo katika, uhamiaji. Mjadala huo unazingatia kanda sita za ulimwengu, yaani Afrika, Asia, Ulaya, Amerika ya Kusini na Karibiani, Amerika ya Kaskazini na Oceania.  Kwa kila mojawapo ya kanda hizi, uchambuzi unahusisha:  

  1. Muhtasari na majadiliano mafupi ya takwimu muhimu zinazohusiana na idadi ya watu; na 
  1. Maelezo mafupi na dhahiri ya "sifa muhimu na maendeleo" katika uhamiaji katika ukanda huo, yakizingatia data, habari na uchambuzi anuwai, pamoja na ule unaotoka kwa mashirika ya kimataifa, watafiti na wachambuzi. 

Kwa ujumla, sura hiyo inazungumzia tofauti muhimu katika kanda na kanda ndogo mbalimbali, pamoja na uchangamano unaoongezeka katika mienendo ya uhamiaji ulimwenguni. Tofauti hizi na uchangamano (baadhi zikiwa ni mahususi kwa mahali na wakati, huku nyingine zkiwa za kawaida katika kanda zote) zinaibua maswali muhimu na changamoto katika utungaji wa sera za kimataifa na kiulimwengu. Kwa mfano, tofauti za kimsingi katika tajriba na mienendo ya uhamiaji katika kanda zote zinapaswa kufikiriwa wakati wa kujadili mifumo ya utawala inayofaa ili ulimwengu udhibiti uhamiaji wa kimataifa. Pia tofauti zinaweza kuwa na athari ya kutumia mbinu bora na katika kuhakikisha kuwa njia za uongozi zinarekebishwa ili kukidhi mahitaji ya kikanda. Vivyo hivyo, ongezeko la uchangamano katika mienendo ya uhamiaji linaleta changamoto za moja kwa moja kwa wasimamizi wa kitaifa na lina athari muhimu kwa mifumo ya utawala inayofaa zaidi na ushirikiano kati ya nchi mbalimbali. 

Chapter 3 provides a discussion of key regional dimensions of, and developments in, migration. The discussion focuses on six world regions, namely Africa, Asia, Europe, Latin America and the Caribbean, Northern America and Oceania.  For each of these regions, the analysis includes: 

  1. An overview and brief discussion of key population-related statistics; and
  2. Succinct descriptions of “key features and developments” in migration in the region, based on a wide range of data, information and analyses, including from international organizations, researchers and analysts.

Overall, the chapter points to important differences across regions and subregions, as well as growing complexities in migration dynamics around the world. These differences and complexities (some of which are specific to place and time, while others are relatively common across regions) raise important questions and challenges for supranational and global policymaking. For example, fundamental differences in migration experiences and dynamics across regions need to be considered when discussing desirable regimes for the global governance of international migration. Differences can also have implications for applying good practices and in ensuring that governance approaches are tailored to meet regional dimensions. Similarly, growing complexities in migration dynamics create direct challenges for national regulators and have important consequences for the most desirable forms of governance and cooperation across countries.