Original Language
Swahili
ISBN (PDF)
978-92-9268-938-4
Number of Pages
41
Reference Number
PUB2024/012/L/2
Year of Publication
2024
Hide Region
Region
Worldwide
Hide all countries
Country
Worldwide

World Migration Report 2024: Chapter 2 (Swahili)

Ripoti ya Uhamiaji Duniani ya 2024: Uhamiaji na wahamiaji: muhtasari wa hali duniani
Also available in:

Sura hii inatoa muhtasari wa data na mienendo ya kimataifa kuhusu wahamiaji wa kimataifa na uhamiaji wa kimataifa. Pia inatoa mjadala wa makundi fulani ya wahamiaji – yaani wafanyikazi wahamiaji, wanafunzi wa kimataifa, wakimbizi, waomba hifadhi na watu waliohamishwa ndani ya nchi (IDPs) – pamoja na fedha zinazotumwa kimataifa. Zaidi ya hayo, sura hii inaangazia idadi kubwa ya data za kiprogramu za IOM, hasa kuhusu wahamiaji waliopotea, wanaosaidiwa kurudi kwa hiari kwenye nchi zao na kujumuishwa tena katika jamii, utoaji wa makazi mapya na ufuatiliaji wa watu waliohamishwa kutoka kwa makazi yao.

Makadirio ya hivi sasa yanaonyesha kwamba kuna wahamiaji wa kimataifa milioni 281 duniani kote (au 3.6% ya idadi ya watu walio duniani). Huku idadi kubwa ya watu ulimwenguni wakiendelea kuishi katika nchi walimozaliwa, watu wengi zaidi wanahamia nchi zingine, hasa zile zilizo katika ukanda wao. Sababu kuu ya watu kuhama kimataifa ni kazi, na wafanyakazi wahamiaji hujumuisha idadi kubwa ya wahamiaji wa kimataifa duniani, huku wengi wao wakiishi katika nchi zenye mapato ya juu. Ufurushwaji wa kimataifa umefikia kiwango cha juu sana, huku idadi ya waliohamishwa ndani ya nchi ikiwa karibu milioni 71.2 na idadi ya wakimbizi na waomba hifadhi ikiwa milioni 40.7.